Skip to main content

Posts

Showing posts from December, 2017

NINI KIMEMPONZA YANGA MBELE YA MBAO?

Na  Hamza matwany Katika mchezo ambao umepigwa katika uwanja wa ccm kirumba mnamo tarehe 31/12/2017 umezikutanisha timu ambazo zinazidi kuwa na upinzani mkubwa kadri miaka inavyozidi kwenda ni mbao fc vs yanga sc. Katika michezo mitatu mfululizo yanga anapoteza mechi katika uwanja wa ccm kirumba. Hivyo mbao kujivunia historia pekee dhidi ya yanga katika uwanja wake wa nyumbani. Ni nini kimeiponza yanga katika mchezo huo? Moja wa sababu ni kuwakosa wachezaji wake muhimu akiwemo obrey chirwa, ibrahimu migomba ajibu, thaban kamusoko na wengine wengi ambao wamekuwa msaada kwa klabu ya yanga ndani ya mwaka huu. Pia yanga imecheza na timu yenye upinzani mkubwa kwao bila ya kuwa na kocha wao mkuu ambae amepata matatizo ya kifamilia, kwa hiyo timu iliongozwa na kocha msaidizi pengine mbinu za kiufundi zilimshinda katika mchezo huo wa jana. Team chemistry pia ilikosekana kwa wachezaji ambao walicheza katika kikosi hicho kwa mfano abdallah shaibu alipata nafasi ya kuanza katika kikosi...

KUELEKEA MCHEZO KATI YA PSG NA REAL MADRID

  Na Muller Idriss Mnamo tar 11 Dec droo ya michuano ya klabu bingwa barani ulaya maarufu kama Uefa ilifanyika na moja kati ya mchezo ulioamsha hisia za wengi hususani wadau wa mchezo wa soka ni mchezo kati ya wababe wa ufaransa PSG dhidi ya Real Madrid. Japo wengi wanautazama mchezo huu kwa kumpa PSG nafasi kubwa ya kushinda na wachache wakimpa Real Madrid kwa sababu ya historia yake kwenye michuano hii ya uefa. Real madrid ndio mabingwa mara kumi na mbili katika michuano hii huku PSG wakiwa hawajawahi kupata ubingwa wa michuano  hii tangu kuanzishwa kwake.    Hizi timu zimekutana mara 7 tangu kuanzishwa kwa hizi timu huku mara sita (6) kati ya hizo ikiwa ni michuano mbalimbali barani ulaya na mara moja ikiwa ni mechi ya kirafiki (pre_season) Kwa mara ya kwanza timu hizi zilikutana msimu wa mwaka 1992/93 ambapo mchezo wa kwanza Madrid alishinda nyumbani kwa mabao 3_1 na waliporudi Ufaransa, wababe hao wa Hispania walikubali kupokea kichapo cha mabao 4_1 hivyo...