Na Muller Idriss
Mnamo tar 11 Dec droo ya michuano ya klabu bingwa barani ulaya maarufu kama Uefa ilifanyika na moja kati ya mchezo ulioamsha hisia za wengi hususani wadau wa mchezo wa soka ni mchezo kati ya wababe wa ufaransa PSG dhidi ya Real Madrid.
Japo wengi wanautazama mchezo huu kwa kumpa PSG nafasi kubwa ya kushinda na wachache wakimpa Real Madrid kwa sababu ya historia yake kwenye michuano hii ya uefa.
Real madrid ndio mabingwa mara kumi na mbili katika michuano hii huku PSG wakiwa hawajawahi kupata ubingwa wa michuano hii tangu kuanzishwa kwake.
Hizi timu zimekutana mara 7 tangu kuanzishwa kwa hizi timu huku mara sita (6) kati ya hizo ikiwa ni michuano mbalimbali barani ulaya na mara moja ikiwa ni mechi ya kirafiki (pre_season)
Kwa mara ya kwanza timu hizi zilikutana msimu wa mwaka 1992/93 ambapo mchezo wa kwanza Madrid alishinda nyumbani kwa mabao 3_1 na waliporudi Ufaransa, wababe hao wa Hispania walikubali kupokea kichapo cha mabao 4_1 hivyo Real Madrid kuondolewa kwenye michuano hiyo.
Mara ya tatu ni msimu wa mwaka 1994/1995 ambapo mchezo wa kwanza Real Madrid akiwa nyumbani alikubali kichapo cha bao moja kwa bila 1_0 kutoka kwa PSG na waliporudi Ufaransa mchezo ulimalizika kwa sare ya bila kufungana na kukamilisha jumla ya michezo minne.
Mwaka 2015 timu hizo zilikutana katika michuano hii zikiwa zimepangwa kundi moja ambapo mchezo wa kwanza ulimalizika kwa sare ya bila kufungana pale Ufaransa na waliporudi Hispania PSG walikubali kipigo cha bao moja kwa bila (1_0).
Na mara ya mwisho walikutana katika pre season mwaka 2016 na Real madrid ililazwa bao 3 kwa 1
Kwa ujumla wake PSG ameshinda michezo mitatu kati ya 7 waliyokutana na Real madrid akishinda michezo 2 kati ya hiyo 7 na wakitoka sare mara 2.
Ukiachana na Historia hizo tuje kuangalia perfomance ya timu hizi mbili kwa sasa..PSG wapo juu kwenye msimamo wa ligi huku Real madrid wakiwa katika nafasi ya tatu kwenye La liga. Safu ya ushambuliaji ya PSG ikiwajumlisha Neymar,Mbappe na Cavanni imefunga magoli 32 mpaka sasa kwenye league 1 huku ile ya Real Madrid Ronaldo,Isco na Asensio ikiwa imefunga magoli 12 tu kwenye La liga pia safu ya PSG imefunga magoli 16 kwenye Uefa mpka sas na madrid ikiwa imefunga magoli 12
Kwa upande wangu nautazama mchezo huu kama mchezo mmoja mzuri sana ambao dunia itashuhudia historia nyingine ikiwekwa katika soka barani ulaya
Comments
Post a Comment