Hamza matwany
Usiku wa tarehe 10 &11-2018 ulikuwa moja ya siku ambazo timu kutoka SERIE A zimeonyesha kwamba mpira ni dakika 90 kwa mechi moja lakini ni 180 kwenye hatua ya mtoano hasa kwenye Champions league .
Roma na juventus zilionekana timu ambazo mechi zao za marudiano zitakuwa rahisi kutokana na matokeo ambayo waliyapata mechi zao za kwanza Juve alipoteza mechi yake ya kwanza akiwa nyumbani kwa jumla ya goli 3-0 dhidi ya miamba ya jiji la madrid na Roma alifungwa 4-1 pale Nou camp.
Mechi za marudio barcelona alimfuata Roma pale stadio olimpio na Roma alifanikiwa kupata ushindi wa goli 3-0 hivyo kufanya agg 4-4 na goli la ugenini lilimpa nafasi ya kusonga mbele.
madrid alimkaribisha Juventus pale Stadio de bernabeu huku madrid wakimkosa naodha wake sergio ramos na Juventus wakimkosa paul dybala wote hao wakiwekwa nje kwa kadi. lakini juve aliusimamisha usiku kama Roma alivyofanya kwa kumfunga madrid goli 3-1 hivyo kufanya agg 4-3 , kitu ambacho hakikutazamwa na wengi kwenye mechi hiyo kama kitatokea.
Timu toka seria A zimepambana vilivyo na kuonyesha nia ya kwenda hatua inayofuata ila Roma alifanikiwa katika hili, lakini kwa wapenzi wa huu mchezo kuna kitu wamejifunza kutoka kwenye hizi mechi mbili kwamba bado seria A ni moja ya ligi 5 bora kabisa barani ulaya.
Mpira unazidi kutengeneza historia kila kukicha kwa sababu ni mara chache sana kuona hivi vitu vikitokea.
#fightingspirit๐๐๐๐๐๐๐
Comments
Post a Comment