Na Hamza matwany.
Roma usiku wa tarehe 10/7/2018 ameweza kuushangaza ulimwengu kwa kile kitendo cha kumtoa fc Barcelona kwenye hatua ya robo fainali kwa kupindua matokeo ambapo mwanzoni alifungwa goli 4-1 nou camp na kufanikiw Kushinda goli 3-0 pale stadio olimpio jijini Roma.
wapenzi wengi wa mchezo huu hawakumpa nafasi Roma kwenda hatua inayofuata katika michuano hii kwa sababu tu ndo timu pekee ilionekana kama dhaifu kwa timu zilizoingia hatua ya robo fainali.
Roma ambae alipita kwa sharkter donestk kwa changamoto ya goli la ugenini lakini katika makundi alipita katika timu kama chelsea , Atletico Madrid na katika timu hizo kote alipata matokeo yaliyomsaidia kufika katika hatua hizi.
Barcelona waliingia katika mchezo wakiwa na spirit ya kwamba mchezo umeisha toka nou camp ,walicheza kwa kujiamini kwamba hakuna maajabu yoyote yanaweza kutokea kwa vile tu walimchukulia kama mnyonge , huku wakiwa wamesahau kwamba hawajawahi kushinda katika stadio olimpio katika mechi 3 za mwisho akiwa barca kapigwa 2 na katoa sare mechi 1.
Na kama bado timu zitakazoingia hatua ya nusu fainali watamchukulia Roma kama mnyonge ataendelea kuushanga ulimwengu kama alivyofanya katika hatua za makundi, mtoano, mpaka robo fainali na ndio maana hii ikaitwa ligi ya mabingwa maana yake kila mtu ana nafasi ya kufika fainal.
Kwa makala hii barcelona wamepoteza mchezo lakini 50% zikiwa zimesababishwa na Ernesto valvede na 50% zikiwa zimesababishwa na wachezaji.
Tuna cha kujifunza katika hii mechi kwamba usikate tamaa kila kitu kinawezekana.
Comments
Post a Comment