NYOTA WATATU WA KIGENI WAONGEZA MKATABA MNONO YANGA SC:
Katika purukushani za usajili ndani ya vilabu mbalimbali hapa bongo tunaendelea kusikia team mbali mbali zinasajili kwa kasi kweli kweli kama Azam , Simba , Kagera sugar , Singida united na kadhilika ila YANGA Imeonekana kuwa kimya kweny hili swala la usajili na kushtusha baadhi ya mashabiki..... Zilitokea tetesi na kusambaa sana kwenye mitandao kuwa Haruna Hakizimana kiungo number 8 wa Yanga amesaini kandaras ya miaka miwili Simba Sc Lakin sisi tulimpigia simu na kumuhoji akasema hizo taarifa hazina ukweli ni uzushi tuu pia hana mpango wa kuichezea simba kabsa kama akimaliza mkataba wake na YANGA wasipomuongeza ni bora akacheze team za nyumbani kwake (Mimi nitaichezea Yanga mpaka kustaafu soka).....
Sasa basi kwa taarifa iliyopo ni kwamba nyota hao watatu wa kigeni wameongeza mkataba ndan ya club ya YANGA SC...
Haruna Hakizimana Niyonzima : kiungo number 8 maridadi kabsa ndani ya club ya yanga ameongeza mkataba wa miaka miwili msimu wa 2017/2018 kucheza ligikuu ya Tanzania..
Thabani Scara Kamusoko: kiungo number 6 maridadi kabsa ndani ya club ya yanga ameongeza mkataba wa miaka miwili msimu wa 2017/2018 kucheza ligikuu Tanzania..
Obrey Cholla Chirwa: Mshambuliaji maridadi kabsa kutokea Zimbabwe club ya fc platnumz ameongeza mkataba wa miaka miwili huku akiwa ana mkataba wa mwaka mmoja msimu huu 2017/2018 bado ataendelea kuichezea yanga Tanzania..
Pia taarifa zilizopo ni kwamba Donald ngoma, Amiss Tambwe na Vicent Bossou hawajataka kuongeza mkataba ndani ya club ya Young Africans ....
Lakin kwa upande wa wazawa wachezaji wengi wameongeza mkataba ila inasemeka alieongeza mkataba mnono zaidi ni beki number 4 wa club hiyo na captain wa team "Nadir Haroub Ally" almaarufu kama Cannavaro yey ametia kandarasi ya miaka mitatu kuendelea kuichezea yanga tangu ajiunge na club hiyo mwaka 2006 kutokea Zanzibar mpak sasa ana miaka 11 jangwani......
Comments
Post a Comment