Hamza matwany
Klabu ya barcelona rasmi imemuachia mchezaji wake arda turan kwa mkopo kwenye klabu ya Bàsàkséhīr ya nchini uturuki.
Arda turan 30 atakuwa kwa mkopo wa miaka 2 na nusu katika klabu hiyo na baada ya hapo barcelona wanaweza kumuuza kwenye klabu yoyote ya ulaya na pia kwenye mkataba wake wa mkopo kuna kipengele cha mkopo ambacho kinawaruhusu instabul basaksehir kumnunua kwa jumla baada ya muda huo wa mkopo na rasmi jana ametambulishwa kwenye klabu hiyo ya uturuki.
Barca walimnunua arda turan kutoka atletico madrid akiwa kwenye kiwango kizuri sana lakini mambo hayakumuendea sawa akiwa na fc barcelona
Arda turan aliandamwa na majeruhi ya muda mrefu katika club hiyo hali iliyomfanya akose nafasi ya kucheza katika klabu hiyo.
Arda turan amedumu katika ligi kuu spain kwa misimu sita na ameshinda la liga, europa league .
Alijiunga na atletico madrid akitokea klabu ya galatasaray ya nchini kwao uturuki, pia likiwa zao ya galatasaray youth academy.
Comments
Post a Comment