Hamza matwany
Kuelekea mchezo wa real socieded dhidi ya barcelona leo katika uwanja wa nyumbani wa real socieded Anoeta stadium, hizi ni takwimu chache kabla ya mchezo huo
Barcelona wanaongoza ligi kwa point 48 huku real socieded wakiwa nafasi ya 13 kwa point 23 katika michezo 18.
Kwenye mechi 7 za mwisho za la liga katika uwanja wa anoeta barcelona hawajawahi kushinda mchezo hata mmoja kati ya hiyo wamefungwa michezo 5 na kutoa sare mara mbili.
Mara ya mwisho barcelona kumfunga real socieded katika uwanja wake wa nyumbani ilikuwa mwaka 2007 katika ushindi wa goli 2_0
Mpaka sasa kwenye mechi 6 za mwisho za ligi real socieded ajashinda mchezo wowote amefungwa michezo 3 na kutoa sare michezo 3 msimu huu
Barcelona hajaruhusu goli lolote katika mechi zake 4 za mwisho za laliga msimu huu mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa may 2016.
Real socieded wamefunga magoli 6 katika dakika 15 za mwanzo kwenye la liga msimu huu.
Messi ndo kinara wa magoli kwenye mechi hii akiwa amefunga magoli 14 kati ya michezo 19 aliyocheza dhidi ya real socieded katika mashindano yote. Na kati ya hayo yote magoli 4 tu ndio kafunga kwenye uwanja wa anoeta.
Jordi alba na sergio roberto ndio wachezaji wanaoongoza kumpa assist mchezaji mmoja kila mmoja akifanya hivyo mara 5
Jordi alba vs messi
Sergio roberto vs suarez.
Ernesto valvede kocha wa barcelona ameshinda mara 5 katoa sare mara 6 kafungwa mara 4 katika awamu zote 15 ambazo amecheza dhidi ya real socieded.
LEO NINI KITATOKEA?
Comments
Post a Comment