Hamza matwany
Weekend hii kutakuwa na kati ya zile mechi kubwa kwenye vodacom premier league( vpl) kati ya wenyeji azam fc mabingwa wa afrika mashariki na kati ikikutana na mabingwa wa kihistoria wa ligi hyo yanga sc.
Ushindani wa yanga na azam unatenganishwa na goli moja na ushindi wa mechi moja kati yao
Yanga na azam zimekutana mara 18 kwenye vpl tangu zilipokutana kwa mara kwanza mwaka 2008 katika mechi hizo yanga amefanikiwa kushinda mechi 6 na azam ameshinda mara 5 huku wakitoka sare michezo 7.
Katika mechi hizo yanga amefunga magoli 26 na azam amefunga magoli 25.
Kwenye mashindano yote ambayo azam na yanga wamekutana takwimu zao ni kama ifuatavyo;
Wamekutana mara 31 yanga ameshinda mara 12 na azam ameshinda mara 11 huku wakiwa wametoka sare mara 8.
Huku yanga akiifunga magoli 41 na azam fc wakiwa wamefunga magoli 40.
UBORA WA VIKOSI VYAO KWA SASA
Kwa msimu huu azam amekuwa na matokeo mazuri katika vpl akiwa ajapoteza mchezo hata mmoja wa ligi na yupo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi.
Azam ndio mabingwa wa mapinduzi cup mwaka 2018. Amekuwa na mwendelezo mzuri ukilinganisha na yanga msimu huu ambayo ikiwa ipo nafasi ya 3 ikiwa imepoteza mchezo 1 dhidi ya mbao.
Yanga kuelekea mchezo huo watawakosa wachezaji wake saba muhimu ; yohana mkomola, abdallah shaibu, amissi tambwe, kamusoko, ngoma,pato ngonyani pamoja na pius buswita kwa sababu wote wanaumwa, licha ya kuumwa buswita anatumikia adhabu yake ya kadi 3 za njano.
#TUKUTANE CHAMAZI COMPLEX
Comments
Post a Comment