Na Muller Idriss
Wakati michezo mbalimbali inaendelea kupigwa katika viwanja mbalimbali nchini Uingereza ikiwa ni muendelezo wa ligi kuu ya nchi hiyo maarufu kama EPL, Fahamu mambo kadha wa kadha kuhusiana na ligi hiyo:-
Manchester United ndiyo timu iliyotwaa ubingwa wa ligi hyo mara nyingi kuliko timu yoyote nchini humo.Imetwaa ubingwa wa ligi hiyo mara 13 tangu mwaka 1992.
Lakini pia Man united ndio timu timu iliyoweka rekodi ya kutwaa ubingwa huo mara tatu mfululizo mnamo msimu wa mwaka 1998-99,199-2000 na 2000-2001 na waliifikia rekodi yao wenyewe mnamo mwaka 2006-07,2007-08 na 2008-09
Rekodi nyingine ni ya kutwaa ubingwa wa epl kwa tofauti ya pointi kubwa. Rekodi hiyo inashikiliwa na klabu ya Manchester United ambapo ilitwaa ubingwa huo kwa tofauti ya pointi 18 baada ya kufikisha pointi 91 wakifuatiwa na Arsenal ambao walifikisha pointi 73. Hiyo ikiwa ni tofauti kubwa ya pointi, tofauti ndogo kabisa ni tofauti ya pointi 0 ambayo iliwekwa mwaka 2011-12 ambapo Manchester city na Man united zilifikisha pointi 89 na ubingwa kuamuliwa kwa tofauti ya magoli, hivyo Man city aliibuka bingwa baada ya kuwa na tofauti ya magoli +64 na Man united +56 Hii ilikuwa ni mwaka wa kwanza kwa Ligi hii kuamuliwa kwa tofauti ya magoli.
Rekodi nyingine ni ya USHINDI.
Chelsea inashikilia rekodi ya kushinda michezo mingi kwa msimu ambapo wameshinda michezo 30 kati ya 38 waliyocheza mnamo 2016-17
Na Derby County ndiyo timu iliyoshinda michezo michache zaidi kwenye Ligi hiyo ambapo ilishinda mchezo mmoja (1)tu kati ya 38 waliyocheza mnamo mwaka 2007-08.
Kwa hayo na mengine mengi endelea kutufatilia katika mitandao ya kijamii
Instagram
Chillu_soccer
Muller Idriss
Dondosha comment yako hapa
ReplyDelete