Muller idrisir
Leo tar 10.Feb.2018 ulipigwa mchezo baina ya timu mbili zinazopatikana Kaskazini mwa jiji la London (Northern London derby). Mchezo huo ulizikutanisha timu za Tottenharm hotspurs na Asernal. Mchezo uliomalizika kwa timu ya Spurs kupata ushindi wa bao moja na sifuri. Hizi ni rekodi mbalimbali kuhusiana na mchezo huo uliomalizika majira ya jioni:
1. Huu ndio mchezo ulioongoza kuhudhuriwa na mashabiki wengi kuliko michezo yote ya Ligi hiyo. Mechi hiyo ilihudhuriwa na watazamaji 83,222 na kuvunja rekodi ya mchezo kati ya Spurs na Man united uliopigwa Mwisho wa juma lilipita ambao ulihudhuriwa na watu 81,978
2.Arsenal wamefungwa kwa mara ya kwanza katika uwanja wa Wembley baada ya kucheza michezo tisa (9) bila kufungwa katika uwanja huo
3. Pia Arsenal wameendelea na rekodi yao ya kutopata ushindi dhidi ya timu 5 za juu wawapo ugenini kwenye Epl baada ya kucheza michezo kumi na tano (15) bila ushindi na leo ni ya 16 bila ya ushindi. Mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 2015 walipowafunga Manchester city mabao 2_0
Comments
Post a Comment