Skip to main content

JANJA JANJA ZA CONTE ZINAVYOIKWAMISHA CHELSEA


Hamzamatwany.
Msimu uliopita timu ya chelsea ilikuwa moja ya club bora kwenye ligi ya EPL lakini hali imekuwa tofauti katika msimu huu. :
Lakini haya matokeo ambayo si yakuridhisha kwenye club hiyo yameletwa na antonio conte ambae ni manager wa miamba hiyo ya darajani

BAADHI YA VITU ALIVYOFANYA. :
Antonie conte alimuachia diego costa ambae alikuwa top score kwa msimu ulioisha kwa ngazi ya club yake na kutimkia atletico madrid, na mbadala wake alifanikiwa kumsajili @alvaromorata  kutoka madrid ili kuziba pengo hilo lakini hali imekuwa tofauti kwenye performances ,Alvaro morata ameshindwa kuziba pengo la costa. :
katika usajili wa mwezi januari alimnunua @oliviergiroudofficial kutoka arsenal ili kusaidiana kuziba pengo hilo lakini bado haijawezekna, alimsajili pia kiungo mshambuliaji @rossbarkley lakini mpka sasa mchezaji huyo ajatumika kwenye club hiyo. :

Antonio conte anataka kuuaminisha ulimwengu kwamba  @davidluiz_4 na @garyjcahill  si mabeki wazuri mbele ya @andreaschristensen3 na  ludiger Hapana ila janja janja zake ndo zinaiponza timu. pia alimsajili @Emerson kutoka Roma lakini hajatumika kwenye club hiyo mpaka sasa :

Antonio conte alimuuza matic kwenda manchester united na alimsajili @bakayoko_official14 kutoka monaco kuwa mbadala wake ila mpaka sasa hajafanikiwa kuziba pengo hilo na pia hata @dannydrinkwater ameshindwa kuvaa viatu vya matic. :

Any way conte anastahili kuwajibika na chelsea alipoifikisha

Comments

Popular posts from this blog

JEZI YA NYUMBANI YA BARCELONA MSIMU WA 2018/2019 IMEVUJA MTANDAONI

Hamza matwany Jezi ya barcelona ya msimu wa 18/19 ambayo inatengezwa na kampuni ya vifaa vya michezo vya nike imevuja mtandaoni. Jezi hiyo ambayo inafanana na jezi ambayo ilitumiwa na club hiyo mwaka 1998 miaka 20  nyuma imetengezwa katika namna hiyo ili kuenzi legends kwa klabu hiyo Jezi ya nyumbani itakuwa ina wekundu na mistari ya blue na bukta nyeusi pia socks zake ni nyeusi kama inavyoonekana kwenye hizo picha

UNYONGE WA ROMA ULIVYOWAPELEKA SEMI FINAL

Na Hamza matwany. Roma usiku wa tarehe 10/7/2018 ameweza kuushangaza ulimwengu kwa kile kitendo cha kumtoa fc Barcelona kwenye hatua ya robo fainali kwa kupindua matokeo ambapo mwanzoni alifungwa goli 4-1 nou camp na kufanikiw Kushinda goli 3-0 pale stadio olimpio jijini Roma. wapenzi wengi wa mchezo huu hawakumpa nafasi Roma kwenda hatua inayofuata katika michuano hii kwa sababu tu ndo timu pekee ilionekana kama dhaifu kwa timu zilizoingia hatua ya robo fainali. Roma ambae alipita kwa sharkter donestk kwa changamoto ya goli la ugenini lakini katika makundi alipita katika timu kama chelsea , Atletico Madrid na katika timu hizo kote alipata matokeo yaliyomsaidia kufika katika hatua hizi. Barcelona waliingia katika mchezo wakiwa na spirit ya kwamba mchezo umeisha toka nou camp ,walicheza kwa kujiamini kwamba hakuna maajabu yoyote yanaweza kutokea kwa vile tu walimchukulia kama mnyonge , huku wakiwa wamesahau kwamba hawajawahi kushinda katika stadio olimpio katika mechi 3 za mwisho a...

DUNIA YA SOCCER IMEJIFUNZA KITU.

Hamza matwany Usiku wa tarehe 10 &11-2018 ulikuwa moja ya siku ambazo timu kutoka SERIE A zimeonyesha kwamba mpira ni dakika 90 kwa mechi moja lakini ni 180 kwenye hatua ya mtoano hasa kwenye Champions league . Roma na juventus zilionekana timu ambazo mechi zao za marudiano zitakuwa rahisi kutokana na matokeo ambayo waliyapata mechi zao za kwanza Juve alipoteza mechi yake ya kwanza akiwa nyumbani kwa jumla ya goli 3-0 dhidi ya miamba ya jiji la madrid na Roma alifungwa 4-1 pale Nou camp. Mechi za marudio barcelona alimfuata Roma pale stadio olimpio na Roma alifanikiwa kupata ushindi wa goli 3-0 hivyo kufanya agg 4-4 na goli la ugenini lilimpa nafasi ya kusonga mbele. madrid alimkaribisha Juventus pale Stadio de bernabeu huku madrid wakimkosa naodha wake sergio ramos na Juventus wakimkosa paul dybala wote hao wakiwekwa nje kwa kadi. lakini juve aliusimamisha usiku kama Roma alivyofanya kwa kumfunga madrid goli 3-1 hivyo kufanya agg 4-3 , kitu ambacho hakikutazamwa na wengi kweny...