Skip to main content

FURAHA JANGWANI

NYOTA WATATU WA KIGENI WAONGEZA MKATABA MNONO YANGA SC:

Katika purukushani za usajili ndani ya vilabu mbalimbali hapa bongo tunaendelea kusikia team mbali mbali zinasajili kwa kasi kweli kweli kama Azam , Simba , Kagera sugar , Singida united na kadhilika ila YANGA Imeonekana kuwa kimya kweny hili swala la usajili na kushtusha baadhi ya mashabiki..... Zilitokea tetesi na kusambaa sana kwenye mitandao kuwa Haruna Hakizimana kiungo number 8 wa Yanga  amesaini kandaras ya miaka miwili Simba Sc Lakin sisi tulimpigia simu na kumuhoji akasema hizo  taarifa hazina ukweli ni uzushi tuu pia hana mpango wa kuichezea simba kabsa kama akimaliza mkataba wake na YANGA wasipomuongeza ni bora akacheze team za nyumbani kwake (Mimi nitaichezea Yanga mpaka kustaafu soka).....

Sasa basi kwa taarifa iliyopo ni kwamba nyota hao watatu wa kigeni wameongeza mkataba ndan ya club ya YANGA SC...

Haruna Hakizimana Niyonzima : kiungo number 8 maridadi kabsa ndani ya club ya yanga ameongeza mkataba wa miaka miwili msimu wa 2017/2018 kucheza ligikuu ya Tanzania..

Thabani Scara Kamusoko: kiungo number 6 maridadi kabsa ndani ya club ya yanga ameongeza mkataba wa miaka miwili msimu wa 2017/2018 kucheza ligikuu Tanzania..

Obrey Cholla Chirwa: Mshambuliaji maridadi kabsa kutokea Zimbabwe club ya fc platnumz ameongeza mkataba wa miaka miwili huku akiwa ana mkataba wa mwaka mmoja msimu huu 2017/2018 bado ataendelea kuichezea yanga Tanzania..

Pia taarifa zilizopo ni kwamba Donald ngoma, Amiss Tambwe na Vicent Bossou hawajataka kuongeza mkataba ndani ya club ya Young Africans ....

Lakin kwa upande wa wazawa wachezaji wengi wameongeza mkataba ila inasemeka alieongeza mkataba mnono zaidi ni beki number 4 wa club hiyo na captain wa team "Nadir Haroub Ally" almaarufu kama Cannavaro yey ametia kandarasi ya miaka mitatu kuendelea kuichezea yanga tangu ajiunge na club hiyo mwaka 2006 kutokea Zanzibar mpak sasa ana miaka 11 jangwani......

Comments

Popular posts from this blog

NINI KIMEMPONZA YANGA MBELE YA MBAO?

Na  Hamza matwany Katika mchezo ambao umepigwa katika uwanja wa ccm kirumba mnamo tarehe 31/12/2017 umezikutanisha timu ambazo zinazidi kuwa na upinzani mkubwa kadri miaka inavyozidi kwenda ni mbao fc vs yanga sc. Katika michezo mitatu mfululizo yanga anapoteza mechi katika uwanja wa ccm kirumba. Hivyo mbao kujivunia historia pekee dhidi ya yanga katika uwanja wake wa nyumbani. Ni nini kimeiponza yanga katika mchezo huo? Moja wa sababu ni kuwakosa wachezaji wake muhimu akiwemo obrey chirwa, ibrahimu migomba ajibu, thaban kamusoko na wengine wengi ambao wamekuwa msaada kwa klabu ya yanga ndani ya mwaka huu. Pia yanga imecheza na timu yenye upinzani mkubwa kwao bila ya kuwa na kocha wao mkuu ambae amepata matatizo ya kifamilia, kwa hiyo timu iliongozwa na kocha msaidizi pengine mbinu za kiufundi zilimshinda katika mchezo huo wa jana. Team chemistry pia ilikosekana kwa wachezaji ambao walicheza katika kikosi hicho kwa mfano abdallah shaibu alipata nafasi ya kuanza katika kikosi...

DUNIA YA SOCCER IMEJIFUNZA KITU.

Hamza matwany Usiku wa tarehe 10 &11-2018 ulikuwa moja ya siku ambazo timu kutoka SERIE A zimeonyesha kwamba mpira ni dakika 90 kwa mechi moja lakini ni 180 kwenye hatua ya mtoano hasa kwenye Champions league . Roma na juventus zilionekana timu ambazo mechi zao za marudiano zitakuwa rahisi kutokana na matokeo ambayo waliyapata mechi zao za kwanza Juve alipoteza mechi yake ya kwanza akiwa nyumbani kwa jumla ya goli 3-0 dhidi ya miamba ya jiji la madrid na Roma alifungwa 4-1 pale Nou camp. Mechi za marudio barcelona alimfuata Roma pale stadio olimpio na Roma alifanikiwa kupata ushindi wa goli 3-0 hivyo kufanya agg 4-4 na goli la ugenini lilimpa nafasi ya kusonga mbele. madrid alimkaribisha Juventus pale Stadio de bernabeu huku madrid wakimkosa naodha wake sergio ramos na Juventus wakimkosa paul dybala wote hao wakiwekwa nje kwa kadi. lakini juve aliusimamisha usiku kama Roma alivyofanya kwa kumfunga madrid goli 3-1 hivyo kufanya agg 4-3 , kitu ambacho hakikutazamwa na wengi kweny...

KOCHA WA STARS ATANGAZA KIKOSI CHA COSAFA

Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Shabani Mayanga,  Jumatano Juni 14, 2017 ametangaza majina ya wachezaji 22 watakaounda kikosi kinachokwenda kushindana kuwania Kombe la Castle Cosafa nchini Afrika Kusini. Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti, inatarajiwa kuanza kambi rasmi kesho Jumapili Juni 18, mwaka huu. Kambi hiyo itakuwa kwenye Hoteli ya Urban Rose, iliyoko Mtaa wa Jamhuri katikati ya jiji la Dar es Salaam. Taifa Stars inajiandaa na michuano ya Cosafa inayotarajiwa kuanza Juni 25, mwaka huu. Michuano hiyo, inaandaliwa na Baraza la Mpira wa Miguu la nchi za Kusini mwa Afrika ambako Tanzania – mwanachama wa Cecafa, imepata mwaliko kushiriki. Tanzania imepangwa kundi A ambako wapinzani wake ni Mauritius, Malawi na Angola wakati Kundi B ni Msumbiji, Shelisheli, Madagascar na Zimbabwe. Timu za Botswana, Zambia na Afrika Kusini kadhalika Namibia, Lesotho na Swaziland zitakuwa na mechi maalumu (play off) ili kuingia robo fainali. Kwa mujibu wa Mayanga...