Skip to main content

RONALDO NA KASHFA KAMA YA MESSI

Unakumbuka ile kesi ambayo ilimkumba Lioneil Messi na mamlaka za mapato za nchini Hispania hadi akapigwa faini ya euro 2m pamoja na kifungo cha nje? sasa kesi ile imehamia kwa mpinzani mkubwa wa Messi ambaye ni Cristiano Ronaldo.

Taarifa zinasema kwa muda sasa toka mwaka 2011 hadi 2014 nyota huyo wa timu ya Real Madrid amekuwa akikwepa kulipa kodi ambapo zaidi ya kiasi cha kodi cha euro 14m amekwepa kulipa katika kipindi hicho.

Tofauti na Lioneil Messi lakini kwa Ronaldo kosa lake ni kubwa sana kwani wapelelezi wa kesi yake wanadai mshambuliaji huyo alifungua hadi kampuni kwa jina jipya ili kukwepa kulipa kodi na kiasi ambacho Ronaldo amekwepa ni mara 3 ya kile kilichomtia Lioneil Messi matatani.

Messi kesi yake ilikuwa ni ukwepaji wa kodi kiasi cha euro 4.1m huku Cristiano Ronaldo ikiwa ni euro 16m, na Messi na baba yake walihukumiwa adhabu ya miezi 21 na faini ya euro 2m hali inayoonesha Ronaldo anaweza kukabiliwa na adhabu kubwa zaidi.

Ronaldo mwenyewe akizungumzia tukio hilo nchini kwao Ureno alipoulizwa na waandishi wa habari alijibu “Quien no debe no teme” akimaanisha “asiye na kitu cha kuficha hawezi kuogopa chochote” na akisisitiza haogopi kitu na ana uhakika wa kushinda kesi hiyo.

Sheria za masuala ya kodi nchini Hispania zinaweza kumuokoa Ronaldo asiende jela kwani kama hujawahi kupata kesi ya kulipa kodi hapo mwanzo au hujawahi kwenda jela na ikiwa ni mara yako ya kwanza kupata kesi kama hiyo baasi unatumikia kifungo cha nje ya jela.

Comments

Popular posts from this blog

JEZI YA NYUMBANI YA BARCELONA MSIMU WA 2018/2019 IMEVUJA MTANDAONI

Hamza matwany Jezi ya barcelona ya msimu wa 18/19 ambayo inatengezwa na kampuni ya vifaa vya michezo vya nike imevuja mtandaoni. Jezi hiyo ambayo inafanana na jezi ambayo ilitumiwa na club hiyo mwaka 1998 miaka 20  nyuma imetengezwa katika namna hiyo ili kuenzi legends kwa klabu hiyo Jezi ya nyumbani itakuwa ina wekundu na mistari ya blue na bukta nyeusi pia socks zake ni nyeusi kama inavyoonekana kwenye hizo picha

KOCHA WA STARS ATANGAZA KIKOSI CHA COSAFA

Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Shabani Mayanga,  Jumatano Juni 14, 2017 ametangaza majina ya wachezaji 22 watakaounda kikosi kinachokwenda kushindana kuwania Kombe la Castle Cosafa nchini Afrika Kusini. Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti, inatarajiwa kuanza kambi rasmi kesho Jumapili Juni 18, mwaka huu. Kambi hiyo itakuwa kwenye Hoteli ya Urban Rose, iliyoko Mtaa wa Jamhuri katikati ya jiji la Dar es Salaam. Taifa Stars inajiandaa na michuano ya Cosafa inayotarajiwa kuanza Juni 25, mwaka huu. Michuano hiyo, inaandaliwa na Baraza la Mpira wa Miguu la nchi za Kusini mwa Afrika ambako Tanzania – mwanachama wa Cecafa, imepata mwaliko kushiriki. Tanzania imepangwa kundi A ambako wapinzani wake ni Mauritius, Malawi na Angola wakati Kundi B ni Msumbiji, Shelisheli, Madagascar na Zimbabwe. Timu za Botswana, Zambia na Afrika Kusini kadhalika Namibia, Lesotho na Swaziland zitakuwa na mechi maalumu (play off) ili kuingia robo fainali. Kwa mujibu wa Mayanga...

DEMBELE OUT WIKI 4

Hamza matwany Madaktari wa klabu ya barcelona wamethibitisha osmanè dembele raia wa ufaransa atakuwa nje kwa wiki 3 hadi 4 kutokana na majeraha ya msuli ambayo aliyapata kwenye mechi dhidi ya real socieded kwenye uwanja wa anoeta jumapili Mchezaji huyo akiwa ametoka kwenye majeraha ya muda mrefu baada ya kukaa nje kwa miezi minne tangu alipoumia mwezi wa nane kwenye mechi dhidi ya getafe. Madaktari wa klabu wamethibitisha majeraha hayo hayata athiri lile jeraha lake la kwanza la upasuaji alilofanya mwezi wa 8 Bado osmane dembele ajakuwa na wakati mzuri kutokana na majehara hayo yanamsumbua.