Na Hamza matwany
Katika mchezo ambao umepigwa katika uwanja wa ccm kirumba mnamo tarehe 31/12/2017 umezikutanisha timu ambazo zinazidi kuwa na upinzani mkubwa kadri miaka inavyozidi kwenda ni mbao fc vs yanga sc.
Katika michezo mitatu mfululizo yanga anapoteza mechi katika uwanja wa ccm kirumba. Hivyo mbao kujivunia historia pekee dhidi ya yanga katika uwanja wake wa nyumbani.
Ni nini kimeiponza yanga katika mchezo huo? Moja wa sababu ni kuwakosa wachezaji wake muhimu akiwemo obrey chirwa, ibrahimu migomba ajibu, thaban kamusoko na wengine wengi ambao wamekuwa msaada kwa klabu ya yanga ndani ya mwaka huu.
Pia yanga imecheza na timu yenye upinzani mkubwa kwao bila ya kuwa na kocha wao mkuu ambae amepata matatizo ya kifamilia, kwa hiyo timu iliongozwa na kocha msaidizi pengine mbinu za kiufundi zilimshinda katika mchezo huo wa jana.
Team chemistry pia ilikosekana kwa wachezaji ambao walicheza katika kikosi hicho kwa mfano abdallah shaibu alipata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza kwenye ligi kuu tangu asajilie kwa hiyo hapakuwa na chemistry mzuri kati yake na andrew vicent hivyo walimfanya Habibu kiyombo kuwa shujaa katika eneo hilo na mchezo wote kwa ujumla.
Pia katika nafasi ya ushambuliaji Amis tambwe aliongoza mashambulizi ya yanga huku akiwa ndo mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu tangu arudi katika majeraha yake, hivyo hakuweza kuleta usumbufu mkubwa na ilikuwa kazi rahisi kwa ulinzi wa mbao kumzuia ikiongozwa na yusuf ndikumana.
Pia katika nafasi ya mashabiki mbao huwa wanakuwa na advantage kubwa ya mashabiki wenye morali kwenye michezo yao dhidi ya timu kubwa zinapofika ccm kirumba.
Comments
Post a Comment