Skip to main content

MAJERAHA MAKUBWA LIGI 5 KUBWA BARANI ULAYA

Hamza matwany
Hivi unawajua wachezaji waliowahi kupata majeraha makubwa na kukaa nje siku nyingi pia kukosa michezo mingi kwenye vilabu vyao?

Nmekuletea hizi takwimu za wachezaji wa ligi kubwa 5 barani ulaya kwa idadi ya majeraha waliyoyapata, siku walizokaa mpaka kupona hayo majeraha yote na michezo pia ambayo wameikosa.

Premier league( EPL)
Kwa upande wa ligi kuu kijana mwenye kipaji kikubwa raia wa uingereza na klabu ya arsenal Jack wilshere ndio anaongoza kwenye ligi hii akiwa amepata majeraha mara 13 akiwa ametumia siku 1013 kuuguza majeraha hayo yote .Jack wilshere amekosa michezo 155 mpaka sasa kipindi chote alichoapata majeraha hayo.

La liga (santander)
Kwenye ligi hii Thomas vermalein mchezaji wa fc barcelona pamoja na taifa ya ubelgiji ndio anaeongoza kwa majeraha mengi kwenye ligi hii akiwa ameumia mara 23 akiwa ametumia siku 1026 katika kuuguza majeraha yote ambayo ameyapata akiwa amekosa michezo 128 katika kipind chote cha majeraha.

Bundersliga
Kwenye ligi kuu ujerumani marco reus wa klabu ya dortmund na taifa la ujerumani ndio anaongoza kwa majeraha mengi zaidi akiwa ameumia mara 41 akiwa ametumia siku 813 kuuguza yote hayo ,huku akiwa amekosa michezo 104 akiwa katika kipindi hicho kigumu.

Seria A
Giuseppe rossi raia wa italy na klabu ya genoa ndio anaongoza kwenye ligi hii akiwa ameumia mara 7 akitumia siku 1194 kuuguza mjeraha hayo huku akiwa amekosa michezo 148 katika kipindi hicho chote.

Ligue 1
Katika ligi kuu nchini ufaransa mchezaji wa marseille na taifa la ufaransa Abou diaby ndio anaongoza akiwa ameumia mara 21 akitumia siku 2072 kuuguza majeraha hayo yote akiwa amekosa mechi 368 katika kipindi chote cha maisha yake ya soka.
Pengine ndio akawa mchezaji wa kwanza mwenye majeraha hatari ya soka kwenye ligi hizi

Comments

Popular posts from this blog

NINI KIMEMPONZA YANGA MBELE YA MBAO?

Na  Hamza matwany Katika mchezo ambao umepigwa katika uwanja wa ccm kirumba mnamo tarehe 31/12/2017 umezikutanisha timu ambazo zinazidi kuwa na upinzani mkubwa kadri miaka inavyozidi kwenda ni mbao fc vs yanga sc. Katika michezo mitatu mfululizo yanga anapoteza mechi katika uwanja wa ccm kirumba. Hivyo mbao kujivunia historia pekee dhidi ya yanga katika uwanja wake wa nyumbani. Ni nini kimeiponza yanga katika mchezo huo? Moja wa sababu ni kuwakosa wachezaji wake muhimu akiwemo obrey chirwa, ibrahimu migomba ajibu, thaban kamusoko na wengine wengi ambao wamekuwa msaada kwa klabu ya yanga ndani ya mwaka huu. Pia yanga imecheza na timu yenye upinzani mkubwa kwao bila ya kuwa na kocha wao mkuu ambae amepata matatizo ya kifamilia, kwa hiyo timu iliongozwa na kocha msaidizi pengine mbinu za kiufundi zilimshinda katika mchezo huo wa jana. Team chemistry pia ilikosekana kwa wachezaji ambao walicheza katika kikosi hicho kwa mfano abdallah shaibu alipata nafasi ya kuanza katika kikosi...

DUNIA YA SOCCER IMEJIFUNZA KITU.

Hamza matwany Usiku wa tarehe 10 &11-2018 ulikuwa moja ya siku ambazo timu kutoka SERIE A zimeonyesha kwamba mpira ni dakika 90 kwa mechi moja lakini ni 180 kwenye hatua ya mtoano hasa kwenye Champions league . Roma na juventus zilionekana timu ambazo mechi zao za marudiano zitakuwa rahisi kutokana na matokeo ambayo waliyapata mechi zao za kwanza Juve alipoteza mechi yake ya kwanza akiwa nyumbani kwa jumla ya goli 3-0 dhidi ya miamba ya jiji la madrid na Roma alifungwa 4-1 pale Nou camp. Mechi za marudio barcelona alimfuata Roma pale stadio olimpio na Roma alifanikiwa kupata ushindi wa goli 3-0 hivyo kufanya agg 4-4 na goli la ugenini lilimpa nafasi ya kusonga mbele. madrid alimkaribisha Juventus pale Stadio de bernabeu huku madrid wakimkosa naodha wake sergio ramos na Juventus wakimkosa paul dybala wote hao wakiwekwa nje kwa kadi. lakini juve aliusimamisha usiku kama Roma alivyofanya kwa kumfunga madrid goli 3-1 hivyo kufanya agg 4-3 , kitu ambacho hakikutazamwa na wengi kweny...

KOCHA WA STARS ATANGAZA KIKOSI CHA COSAFA

Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Shabani Mayanga,  Jumatano Juni 14, 2017 ametangaza majina ya wachezaji 22 watakaounda kikosi kinachokwenda kushindana kuwania Kombe la Castle Cosafa nchini Afrika Kusini. Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti, inatarajiwa kuanza kambi rasmi kesho Jumapili Juni 18, mwaka huu. Kambi hiyo itakuwa kwenye Hoteli ya Urban Rose, iliyoko Mtaa wa Jamhuri katikati ya jiji la Dar es Salaam. Taifa Stars inajiandaa na michuano ya Cosafa inayotarajiwa kuanza Juni 25, mwaka huu. Michuano hiyo, inaandaliwa na Baraza la Mpira wa Miguu la nchi za Kusini mwa Afrika ambako Tanzania – mwanachama wa Cecafa, imepata mwaliko kushiriki. Tanzania imepangwa kundi A ambako wapinzani wake ni Mauritius, Malawi na Angola wakati Kundi B ni Msumbiji, Shelisheli, Madagascar na Zimbabwe. Timu za Botswana, Zambia na Afrika Kusini kadhalika Namibia, Lesotho na Swaziland zitakuwa na mechi maalumu (play off) ili kuingia robo fainali. Kwa mujibu wa Mayanga...