Skip to main content

NAMFAHAMU VIZURI ABRAMOVICH CONTE JIANDAE

Hamza matwani
chelsea ni moja ya club duniani zinazomilikiwa na mtu binafsi ambae ni Roman abramovich , lakini boss huyo anatambulika kwa kutoweza kumvulia kocha ikiwa timu inapata matokeo mabaya japo kwa msimu mmoja :

Antonio conte anakuwa kocha wa 16 kuifundisha chelsea toka mwaka 2000 kwa wastani kila kocha amedumu kwenye club hiyo kwa mwaka mmoja na mwezi mmoja. :

makocha mashughuli duniani wamepita kwenye club hiyo tangu mwaka 2000 mfano josë mourinho, fellipe scolari, claudio ranieri, Rafa benitez, Guus huddink, Andre villa boas, carlo anceloti, steve holland, ray wilkins , Roberto di mateo na wengine wengi. :  Antonio conte mkataba wake unamalizika mwaka 2021 lakini sitarajii kuona akimaliza mkataba huo kwa muda husika bila kutupiwa vilago vyako. :

unamkumbuka Roberto di mateo kocha pekee aliewapa taji la UEFA club hiyo kwa kupita katika migongo ya timu ngumu duniani akifanya come back ya historia pale darajani kwa kuwafunga napoli jumla ya goli 4-1baada ya kufungwa kwenye first leg na Napoli goli 3 -1.Baadae alifanikiwa kumfunga barcelona na kucheza fainali na Bayern na kupata ubingwa ambao ni historia kwa club. Lakini baada ya mwaka mmoja tu alitimuliwa kwenye club hiyo. :
mpaka sasa sioni sababu ya kusema conte atabaki mpaka mwaka 2021 ikiwa timu inapigania kucheza UEROPA msimu ujao, akitoka kuwa bingwa msimu uliopita , huku akipata matokeo mabaya kwenye mechi za hivi karibuni. :

Amepoteza mchezo dhidi ya barca, katoka kupoteza dhidi ya totnham, na jana tu akitoka kutoa sare na westham nyumbani. :

Sitashangaa kumuona manager mpya akiwa na chelsea msimu ujao kwa sababu tu namfahamu Roman abramovich.

Comments

Popular posts from this blog

JEZI YA NYUMBANI YA BARCELONA MSIMU WA 2018/2019 IMEVUJA MTANDAONI

Hamza matwany Jezi ya barcelona ya msimu wa 18/19 ambayo inatengezwa na kampuni ya vifaa vya michezo vya nike imevuja mtandaoni. Jezi hiyo ambayo inafanana na jezi ambayo ilitumiwa na club hiyo mwaka 1998 miaka 20  nyuma imetengezwa katika namna hiyo ili kuenzi legends kwa klabu hiyo Jezi ya nyumbani itakuwa ina wekundu na mistari ya blue na bukta nyeusi pia socks zake ni nyeusi kama inavyoonekana kwenye hizo picha

KOCHA WA STARS ATANGAZA KIKOSI CHA COSAFA

Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Shabani Mayanga,  Jumatano Juni 14, 2017 ametangaza majina ya wachezaji 22 watakaounda kikosi kinachokwenda kushindana kuwania Kombe la Castle Cosafa nchini Afrika Kusini. Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti, inatarajiwa kuanza kambi rasmi kesho Jumapili Juni 18, mwaka huu. Kambi hiyo itakuwa kwenye Hoteli ya Urban Rose, iliyoko Mtaa wa Jamhuri katikati ya jiji la Dar es Salaam. Taifa Stars inajiandaa na michuano ya Cosafa inayotarajiwa kuanza Juni 25, mwaka huu. Michuano hiyo, inaandaliwa na Baraza la Mpira wa Miguu la nchi za Kusini mwa Afrika ambako Tanzania – mwanachama wa Cecafa, imepata mwaliko kushiriki. Tanzania imepangwa kundi A ambako wapinzani wake ni Mauritius, Malawi na Angola wakati Kundi B ni Msumbiji, Shelisheli, Madagascar na Zimbabwe. Timu za Botswana, Zambia na Afrika Kusini kadhalika Namibia, Lesotho na Swaziland zitakuwa na mechi maalumu (play off) ili kuingia robo fainali. Kwa mujibu wa Mayanga...

DEMBELE OUT WIKI 4

Hamza matwany Madaktari wa klabu ya barcelona wamethibitisha osmanè dembele raia wa ufaransa atakuwa nje kwa wiki 3 hadi 4 kutokana na majeraha ya msuli ambayo aliyapata kwenye mechi dhidi ya real socieded kwenye uwanja wa anoeta jumapili Mchezaji huyo akiwa ametoka kwenye majeraha ya muda mrefu baada ya kukaa nje kwa miezi minne tangu alipoumia mwezi wa nane kwenye mechi dhidi ya getafe. Madaktari wa klabu wamethibitisha majeraha hayo hayata athiri lile jeraha lake la kwanza la upasuaji alilofanya mwezi wa 8 Bado osmane dembele ajakuwa na wakati mzuri kutokana na majehara hayo yanamsumbua.