Hamza matwany Weekend hii kutakuwa na kati ya zile mechi kubwa kwenye vodacom premier league( vpl) kati ya wenyeji azam fc mabingwa wa afrika mashariki na kati ikikutana na mabingwa wa kihistoria wa ligi hyo yanga sc. Ushindani wa yanga na azam unatenganishwa na goli moja na ushindi wa mechi moja kati yao Yanga na azam zimekutana mara 18 kwenye vpl tangu zilipokutana kwa mara kwanza mwaka 2008 katika mechi hizo yanga amefanikiwa kushinda mechi 6 na azam ameshinda mara 5 huku wakitoka sare michezo 7. Katika mechi hizo yanga amefunga magoli 26 na azam amefunga magoli 25. Kwenye mashindano yote ambayo azam na yanga wamekutana takwimu zao ni kama ifuatavyo; Wamekutana mara 31 yanga ameshinda mara 12 na azam ameshinda mara 11 huku wakiwa wametoka sare mara 8. Huku yanga akiifunga magoli 41 na azam fc wakiwa wamefunga magoli 40. UBORA WA VIKOSI VYAO KWA SASA Kwa msimu huu azam amekuwa na matokeo mazuri katika vpl akiwa ajapoteza mchezo hata mmoja wa ligi na yupo nafasi ya pili katik...
Habari zote za michezo duniani kote